Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
jana usiku amekutana na nahodha wa Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa
Stars), Mbwana Samatta huko Ubelgiji alikoenda kwa ajili ya Mkutano wa
kutatua migogoro ya kisiasa nchini Libya.
Mzee Kikwete mapema baada ya kukutana na nyota huyo anayekipiga kunako
Klabu ya Genk alionesha furaha yake na kuandika ujumbe mzuri wa
kufurahishwa kwa kukutana nae.
“Nikiwa hapa Brussels kuhudhuria Mkutano wa Wadau wa Libya nimepata
fursa ya kukutana na mwanasoka na kipenzi chetu @samatta77 leo hii“,
Ameandika Kikwete lwenye ukurasa wake wa Twitter.
Samatta nae hakuchukulia poa shavu hilo la kutembelewa na Rais Mstaafu
kwa Kuandika “Ni wakati mzuri siku zote kukutana na our former president
Mr @JakayaKikwete Wise and charming man. Asante sana mheshimiwa mungu
akuweke” .
Mbwana Samatta ni moja ya wachezaji ambao wametajwa kwenye kikosi cha
Taifa Stars kinachojiandaa kuvaana na Lesotho mwezi ujao kwenye mechi za
kufuzu AFCON.