Utafiti mpya unaonyesha kuwapo kwa uhusiano kati ya unywaji wa pombe
miongoni mwa wanawake na ongezeko la kupata na saratani ya matiti.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka na mfuko wa utafiti wa saratani ni kuwa nusu
glasi ya mvinyo au bia kwa siku huongeza uwezekano wa kupata saratani
ya matiti.
Mbali na hayo, utafiti huo pia unaonesha kuwa mazoezi ya mara kwa mara
huweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi hayo ya saratani.
Inaelezwa kuwa saratani ya matiti ndiyo huwakumba zaidi wanawake nchini
Uingereza huku mmoja kati ya wanawake wanane wakipatwa na ugonjwa huo
katika maisha yao