Ommy Dimpoz awajibu wanaosema anajipendekeza kwa Matajiri. - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Jul 2017

Ommy Dimpoz awajibu wanaosema anajipendekeza kwa Matajiri.

Moja ya story ambazo zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao mbalimbali ni kuhusu Ommy Dimpoz kuitwa chawa akidaiwa kuwaganda baadhi ya watu wenye uwezo kifedha wakifurahi kitu ambacho amekanusha akisema watu wamekuwa wakijadili picha bila kujua ukweli.
Akiwa kwenye XXL ya Clouds FM leo July 6, 2017 Ommy Dimpoz amefunguka baada ya kuulizwa na Mtangazaji kuwa anadaiwa kupiga picha na matajiri akiwa nao pamoja na kuishi maisha ambayo ni expensive.

>>>“Kwenye kujipiga picha inahitaji umakini mkubwa sana kwa sababu picha unazopiga zinaenda mbali sana. Huwezi kuamini sana safari yangu ya IBIZA nilikuwa kwenye show Malindi Kenya mwaliko niliupata toka kwa shabiki yangu. Shakaji aliyenipeleka IBIZA nilimueleza kuhusu mipango yangu ya kazi akani-support katika video yangu ya Kajiandae.

“Nilipokwenda Dubai nilitumia Hashtag ya Hello Dubai nikapata dili Dubai la kutangaza Utalii wa Dubai. Watu wa Utalii wa Dubai walinilipa mkwanja kuweka picha nikiwa Dubai, wakanipa offer ya video pia.” – Ommy Dimpoz.