Barakah The Prince Yamkuta Makubwa...Kina Ali Kiba Wampokonya Account ya Youtube..... - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Aug 2017

Barakah The Prince Yamkuta Makubwa...Kina Ali Kiba Wampokonya Account ya Youtube.....

Barakah The Prince Yamkuta Makubwa...Kina Ali Kiba Wampokonya Account ya Youtube.....
Msanii wa muziki, Barakah The Prince ameanza maisha yake mapya akiwa na label yake ya Bana Music ikiwa ni miezi michache toka aachane na label ya RockStar4000 iliyokuwa ikimsimamia.


Muimbaji huyo ametangaza kufungua akaunti mpya ya YouTube na kuiacha ile ambayo aliyokuwa akiitumia akiwa katika label ya hiyo ya zamani.

Barakah ametoa taarifa kwamba soon atafungua akaunti mpya ya YouTube ambapo kazi zake mpya za muziki zitakuwa zikipatikana kupitia channel hiyo.
 “Ndugu zangu nitawatangazia soon YouTube channel yangu mpya kuna zawadi zenu kama 5 hivi…basi na hii itadondoka ndugu zangu,” aliandika Barakah Instagram.

Label ya RockStar4000 haijawahi kuzungumza chochote toka muimbaji huyo atangaze kung’atuka kwa madai kuwa kuna baadhi ya vitu anaona haviendi sawa.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo ameonekana kuwa katika maandalizi ya kuachia kazi yake ya kwanza akiwa nje ya label hiyo baada ya kuonekana akiwa location akishoot video ya wimbo wake mpya.