“Bill Gate Ameamua Mwenyewe Kutuletea Hizi Fedha Sikumuomba…” – Rais Magufuli - MULO ENTERTAINER

Latest

12 Aug 2017

“Bill Gate Ameamua Mwenyewe Kutuletea Hizi Fedha Sikumuomba…” – Rais Magufuli

Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na tajiri Namba 1 Duniani Bill Gates ambaye kupitia Taasisi yake ya Bill and Melinda Gates ametengea zaidi ya Dola Milioni 350 kuisaidia Tanzania.

 ”Tunamshukuru sana, ameamua mwenyewe kutuletea hizi fedha na anasema tunaenda vizuri. Kwa hiyo ameona hana mahala pa kuzipeleka hizi hela anazileta Tanzania kwa sababu tunajua kuzitumia.

“Hataki hela yake anaihangaikia kule halafu inakuja hapa inatumika ovyo. Tumemueleza hatua zetu na amekuwa akizisikia, anaziona hatua tunazochukua za kupambana na Ufisadi.” – Rais Magufuli.  

VIDEO: