Nani Atafaa Kuogombea Urais kwa Chadema 2020? - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Aug 2017

Nani Atafaa Kuogombea Urais kwa Chadema 2020?


Kwanza niseme binafsi simwitaji EL kuwa mpeperusha bendera ya CHADEMA 2020, ila kama anataka astaafishwe siasa kwa lazima agombee tu.

Ila kwa ujumla naangalia tunavyojipanga na tunavyoenenda ndani ya chama chetu cha CHADEMA, hivi ni nani anaweza kupeperusha bendera yetu 2020?

Ukiangalia kwa macho ya nyama hupati hata mmoja labda itokee kama 2015. Kama Dr. Slaa ambaye tuliamini alikuwa na nguvu ya kuitoa CCM bila jasho kabisa, kwa sasa nani anafikia hata nusu ya Dr. Slaa pale kwetu?

Ni mawazo tu haya.

Hebu tuchangie kwa utulivu.

By Ufipa-Kinondoni