Tambua..Waweza Kuridhia Kufanya Mapenzi Hata Kama Umepoteza Fahamu Ukiwa Umelewa.... - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Aug 2017

Tambua..Waweza Kuridhia Kufanya Mapenzi Hata Kama Umepoteza Fahamu Ukiwa Umelewa....

Tambua..Waweza Kuridhia Kufanya Mapenzi Hata Kama Umepoteza Fahamu Ukiwa Umelewa....
Profesa wa Saikolojia nchini Marekani, mwanamama Kim Fromme ameamua kuthibitisha kwamba sio tu kwa sababu mtu amepoteza fahamu kutokana na ulevi basi iwe hajaridhia kujamiiana.

Amefanya kazi kwa miaka 24 iliyopita kutafiti uhalali wa ridhaa ya kufanya mapenzi anayotoa mtu akiwa amepoteza fahamu kutokana na kuzidiwa na pombe. Jarida la BuzzFeed limeripoti kuwa profesa huyu ameshatoa ushahidi mahakamani, kushauri, au kutoa maelezo ya kitaalamu kwa zaidi ya kesi 50 za jinai, madai na kesi za Kijeshi zinazohusu ubakaji tangu mwaka 2009.

Tafiti zilizoendeshwa na Profesa Fromme zimeonesha kwamba takriban asilimia 50 ya watu wanaokunywa pombe huwa wanapoteza fahamu na ni jambo la kawaida zaidi kutokea kwa wanawake wanaokunywa pombe.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyu, kuna aina mbili za kupoteza kumbukumbu kutokana na ulevi: ya kwanza inatokea ambapo muathirika huwa anakumbuka baadhi tu ya mambo yaliyokuwa yanaendelea akiwa amelewa, lakini sio tukio zima mwanzo hadi mwisho, na ya pili ni pale mtu anapokuwa anaelewa kinachotokea lakini hakihifadhiwi kwenye kumbukumbu ya muda mrefu kwenye ubongo. Kwenye aina ya kwanza, marafiki uliokuwa nao wakati mnaelewa wanaweza kukusaidi kukumbuka matukio uliyoyasahau, lakini kwenye aina ya pili, bila shaka yawezekana usikumbuke jambo lolote lililotokea hata kama ulilifanya, ulifanyiwa au uliruhusu ufanyiwe.

Katika ushahidi wake — kama kwenye kesi ya mwaka 2013 jijini Ohio ambapo wanamichezo wawili walishtakiwa kwa kosa la ubakaji — Fromme alisema kwamba wakati mtu anapopoteza fahamu, bado ubongo wake unaendelea kufanya kazi lakini unakuwa unashindwa kuhifadhi kumbukumbu ya matukio yanayoendelea kwa muda mrefu, lakini ukizimia, ubongo unaacha kabisa kufanya kazi.

Kwenye utetezi wake wa kesi hiyo, Fromme alisema kuwa, “kama ambavyo mwanamke huyu hakumbuki kwamba alibakwa kwa sababu alikuwa amepoteza fahamu, ndio vivyo hivyo ambavyo hawezi kukumbuka kama aliridhia mwenyewe kujamiiana.”

Profesa Fromme bado anatumiwa kutoa ushahidi wake wa kitaalamu kwenye kesi nyingi za unyanyasaji wa kingono na ubakaji unaohusisha walevi ambapo anadai kuwa mtu akipoteza fahamu kutokana na pombe haimaanishi kwamba anapoteza uwezo wa kutoa ridhaa halali ya kujamiiana na mtu. Mwanamama huyu amesema kuwa anaamini kuwa ana wajibu wa kimaadili ya taaluma kuhakikisha anaelimisha jamii kuhusu kupoteza fahamu.