Nina Mimba ya Rafiki wa Mume Wangu, Nifanyeje? - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Sept 2017

Nina Mimba ya Rafiki wa Mume Wangu, Nifanyeje?

Hi guys i hope mko poa,

Nimekuja kwenu kuomba ushauri kwa sababu najua hapa JamiiForums hatujuani tofauti na mitaani.

Mwezi uliopita mpenzi wangu alisafiri kikazi nje ya nchi na hata sasa hajarudi ila yuko mbioni kurudi.

Alipoondoka kama wiki hivi, rafiki yake alikuja kutuona tunaendeleaje, bahati mbaya watoto nilikuwa nimewapeleka kwa mama yangu wakashinde huko weekend yote hiyo, so shemeji alinikuta peke yangu.

Sijui tulianza anzaje, nilikua na feelings kali sana, nilitoa wine tukawa tunakunywa huku tukizungumza mawili matatu, as time went on tukaanza michezo michezo ya kutaniana, nasikitika mwisho wa utani huo kwa bahati mbaya shetani akatupitia tukawa tumezini na baadae tukahamia bedroom.

Hadi sasa tumeshafanya kama mara nane hivi, tumekua pia tuki meet katikati ya wiki, i accept that he is real good than my hubby.

On Tuesday niliamka na homa kali sana kama mtu mwenye Malaria hivi, nikaenda hospital kucheck Malaria but to my surprise naambiwa Niko pregnant, I was shocked, kwa sababu baada ya hubby kusafiri nilipata period, so kwa vyovyote itakuwa ya shemeji.

Nilikuwa najiuliza sijui niitoe kabla hubby hajarudi kwa sababu anarudi ndani ya siku 4 au 5 au nimsubiri aje nimsukumie yeye? Ila pia nina wasiwasi mtoto akija kufanana na shemeji itakuaje?

Nifanyaje?