IGP Simon Sirro amefunguka na kusema kuwa viongozi wastaafu wa jeshi la polisi nchini wamempa ushauri namna ambavyo anapaswa kuendesha jeshi hilo na kudai viongozi hao wameona mapungufu mbalimbali ndani ya jeshi hilo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi.
Akiongea na waandishi wa habari IGP Sirro jana baada ya kumaliza mkutano na wastaafu hao alisema mambo kadhaa ambayo alishauriwa na viongozi hao ambayo jeshi la polisi linatakiwa kulifanyia kazi.
"Jambo kubwa ambalo walikuwa wanasisitiza ni suala la weledi kwamba wanapokuwa kule wanatuangalia sisi ambao tuko jeshini tunahudumia Watanzania wanaona kuna mapungufu katika baadhi ya utendaji wa askari wetu, kwa hiyo walikuwa wanasisitiza sana katika suala la weledi, lakini la pili viongozi hawa wanazungumzia sana suala la mafunzo kwamba kila askari anapaswa kuwa na mafunzo mbalimbali" alisema IGP Sirro
Baadhi ya maafisa wastaafu wa jeshi la polisi walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na IGP Mstaafu Ernest Mangu, saima Mwema, Omari Maita pamoja na makamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleman Kova na Afred Tibaigana
10 Sept 2017
New