BREAKING NEWS: JACOB ZUMA AJIUZURU URAIS WA AFRIKA YA KUSINI. - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Feb 2018

BREAKING NEWS: JACOB ZUMA AJIUZURU URAIS WA AFRIKA YA KUSINI.

Kiongozi mkuu wa chama kikuu cha ANC Rais Jacob Zuma akitangaza kujiuzuru usiku wa leo.
Baada ya shirika la Utangazaji la nchi hiyo, SABC, kutangaza kuwa chama cha ANC kimempatia Zuma masaa 48 kuwa tayari amewasilisha barua yake ya kujiuzulu. Hata hivyo, maafisa wa chama hicho hawakupatikana kuthibitisha taarifa hizo, ingawa chama hicho kimeitisha mkutano na waandishi wa habari baadaye hii leo katika makao makuu ya chama hicho mjini Johannesburg.
Chama cha ANC pia kinaweza kumlazimisha Zuma kujiuzulu lakini mamlaka hayo yanaishia katika ngazi ya chama tu na habanwi na katiba ya nchi hiyo  kulazimika kujiuzulu.