Recho Kizunguzungu Akana Kutoka Kimapenzi na TID "TID Hawezi Kuwa Mtu Wangu" - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Feb 2018

Recho Kizunguzungu Akana Kutoka Kimapenzi na TID "TID Hawezi Kuwa Mtu Wangu"

Recho Akana Kutoka Kimapenzi na TID "TID Hawezi Kuwa Mtu Wangu"


Msanii wa muziki Bongo, Rachel amesema hajawahi kutoka kimapenzi na TID kama inavyokuwa ikiripotiwa.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Same Boy’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na wala hajawahi kubeba ujauzito wa TID.

“Niseme tu TID sio bwana yangu, sio mtu wangu, TID hawezi kuwa mtu wangu, TID mkubwa ujue, ana type zake, mimi nina type zangu za wanaume ambao natakiwa ni date nao, TID siyo type ya wanaume ambao naweza ku-date nao, kirafiki kuongea sawa,” amesema.

“Naomba nieleweke, sijawahi kutoka kimapenzi na TID, sijawahi kubeba mimba ya TID hata mara moja,” amesisitiza Rachel.