Skendo ya Unga Ilivyomtafuna Baby Madaha - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Feb 2018

Skendo ya Unga Ilivyomtafuna Baby Madaha


MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu na muziki Bongo, Baby Madaha ameeleza kuwa katika maisha yake hakuna kitu kilichowahi kumtafuna na kumletea shida kwenye familia yake kama skendo ya kutumia unga.

Baby amesema kuwa, skendo hiyo ilitokana na kushiriki kwenye filamu mbalimbali akiwa kama teja, jambo ambalo lilisababisha watu wazushe kwamba alikuwa akitumia unga.

“Kiukweli skendo ya unga ilinitesa sana kiasi kwamba familia yangu wakajua kweli ninatumia unga, unajua mama yangu na mdogo wangu ni madaktari, kwa hiyo suala hilo lilikuwa ni la aibu kiasi kwamba walinichukua na kunipeleka hospitalini kupima huko ndiko nikagundulika kwamba nilikuwa situmii unga, hiyo ndiyo ikawa nafuu yangu,” alisema Baby Madaha.