Katika kuelekea mchezo maalum wa kukata na shoka wa kujitolea ili kuchangia elimu, mshambuliaji wa timu ya taifa na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta ametangaza kikosi chake kitakachocheza na kile cha Alikiba.
Kwenye kikosi hiko Samatta amewataja mastaa wa zamani na sasa hivi kwenye soka hapa nchini pamoja na mchezaji mahiri wa TP Mazembe, Trésor Mputu, huku msemaji wa timu hiyo akiwa ni mchekeshaji maarufu Joti.
Wachezaji waliotajwa kwenye kikosi hiko ni Juma Kaeja, Kabaly Faraji, Shomari Kapombe, Mohammed Zimbwe, Kelvin Yondani, Nadri Haroub, Athumani Chuji, Haruna Shamte, Mohammed Samatta, Thomas Ulimwngu, Farid Musa, Hruna Boban na Amri Kiemba.
Wengine ni Athumani Machupa, Henry Joseph, Rashid Gumbo, Mrisho Ngasa, Sultan Kaskas, Saleh Jembe na Shaffih Dauda.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 9 ya mwaka huu.
28 May 2018
New