Mike Pence Amuonya Kim Jong-un Asimchezee Trump - MULO ENTERTAINER

Latest

22 May 2018

Mike Pence Amuonya Kim Jong-un Asimchezee Trump

Mike Pence Amuonya Kim Jong-un Asimchezee Trump
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amemuonya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuwa asimchezee Rais Donald Trump ikiwa watakutana mwezi ujao.

"Yatakuwa ni makosa makubwa kwa Kim Jong-un kufikiri kuwa atamchezea Donald trump," Bw Pence alisema wakati akihojiwa na kituo cha Fox News.

Bw Pence pia alisema kuwa Bw Trump anaweza kuondoka kwenye mkutano huo wa Juni 12.

Korea Kaskazini imetisha kujitoa mkutano huo baada ya matamshi ya mshauri wa masuala ya ya ulinzi nchini Marekani John Bolton.

Korea Kaskazini ilijibu vikali walati Bolton alisema kuwa itafuata mfumo wa Libya katika kuondoa zana za nyuklia.