New
Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amemtumia salamu za Birthday njema Msanii mwenzake na rafiki yake Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz.
Siku ya leo ni siku ya kuzaliwa ya Ommy Dimpoz na rafiki yake na mtu wake wa karibu kabisa Ali Kiba kamuwish Birthday njema na ujumbe mzito.
Happy Birthday @ommydimpoz enjoy your special day bro Na wala Usiwaze.Mwenyezi MUNGU ndie Muumbaji Wa wanyonge Na wajanja . Hivyo basi tunatakiwa tumshukuru kwa kutupa/Na Kutunusuru KWASABABU MUNGU Ana maana yake NA anatupenda Sote ..KAZA 💪🏾
#mofayabyalikiba
#KingKiba
Ali Kiba amemtaka asijali sana wala asiyawaze yale magumu aliyopitia Miezi michache iliyopita baada ya kulazwa hospitali kwa Miezi karibia mitano badala yake amshukuru tu Mwenyezi Mungu.
Kwenye posti yake ya leo ya birthday Ommy Dimpoz amemshukuru sana Ali Kiba kwa kuwa naye kipindi chote cha ugonjwa na hata kuweka wazi kuwa amemuuguza.
Ali Kiba alisimamisha kuachia kinywaji chake cha Mofaya Miezi michache iliyopita baada ya kukizindua kutokana na maradhi ya Ommy Dimpoz.