Jay Z Afanikiwa Kumtoa Kileleni P. Didy Kwenye Orodha ya Wenye Pesa Nying - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Sept 2018

Jay Z Afanikiwa Kumtoa Kileleni P. Didy Kwenye Orodha ya Wenye Pesa Nying

Jay Z Afanikiwa Kumtoa Kileleni P. Didy Kwenye Orodha ya Wenye Pesa Nyingi
Rapa mkongwe duniani Jay Z amefanikiwa kumtoa kileleni Sean Combs maarufu kama P. Didy kwenye orodha ya wasanii wa hiphop wanaotengeneza pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2018 kwa kutengeneza dola za kimarekani 76.5 kwa mujibu wa Jarida la kibiashara la Forbes.


P. Diddy aliwahi kuongoza nafasi hiyo ya kwa takribani miaka mitatu mfululizo kulingana na kipato chake alichokuwa ana kitengeneza kupitia kazi zake.

Katika orodha hiyo iliyotolewa na Forbes hakuna rapa wa kike hata mmoja aliyeweza kutusua na kuingia katika mwaka huu.

Wakati jarida la kibiashara la Forbes likitoa orodha hiyo ya rapa wanaotengeneza fedha nyingi duniani kupitia kazi zao, kwa upande wa rapa wa Tanzania bado wapo katika wakati mgumu kutambua thamani halisi wanayotengeneza kwa mwaka hata miezi kutokana na watu hao kufanya mambo yao kiusiri na kudhania kwamba wakitaja viwango vyao huenda wakachekwa au kudharauliwa.