Jose Chameleone Atangaza Rasmi Kuachana na Mkewe - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Jose Chameleone Atangaza Rasmi Kuachana na Mkewe

Jose Chameleone Atangaza Rasmi Kuachana na Mkewe
Inaripotiwa kuwa superstar Jose Chameleone kutokea Uganda ametangaza rasmi kuachana na mke wake Daniella Mayanja  kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka kumi.

Inadaiwa kuwa ndoa hiyo ilionekana kuingia dosari tokea 2017 na kupitia ujumbe aliouandika Jose Chameleone amedai kuwa amechoka kujitetea kila siku na anaamini kuwa wajinga ndio wangefanya hivyo kila siku ila kwa upande wake inatosha.

Jose Chameleone na Daniella walifunga ndoa June 7,2008 na kubahatika kupata watoto wanne na ndoa hiyo imedumu kwa miaka kumi na kuvunjika rasmi September 16,2018 baada ya Jose Chameleone kutangaza .

“Kila kitu kinabidi kiishe,nimeshindwa sikuwa mtu bora kama ilivyotakiwa  kitu gani kingine tunahitaji, Mungu ametubariki, ametupenda na daima tabaki kuwa nasi , watu wapumbavu watahisi ni kitu cha promosheni na wataweka mawazo yao ya kijinga”

“Sipo kwenye mahusiano na sitafuti wa kuwa nae na nitakuwa mwanaume wa mwisho kusimama, nakuacha uwe Daniella Mungu akubariki siku zote ,siwezi kujitetea kila siku wajinga ndio watafanya hivyo”

“Umekuwa kila kitu kwangu lakini inatosha nakutakia kila la kheri, nimeumia roho lakini inabidi nifanye maamuzi”