Kikosi cha Simba kimewasili salama jijini Mwanza kwa ajili ya kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa dhidi ya Mbao FC Alhamis ya wiki hii.
Jumla ya wachezaji 20 wamesafiri na kikosi huku kadhaa wakisalia Dar es Salaam na kuungana na kile cha pili kwa ajili kuendelea kujifua kwa mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.
Wachezaji 20 ambao wametua mwanza ni magolikipa Aishi Manula na Deo Munishi Dida, Shomary Kapombe, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Pascal Wawa na Jonas Mkude.
Wengine ni Clatous Chama, James Kotei, Mohammed Ibrahim, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Shiza Kichuya, Meddie Kagere, John Boko, Emanuel Okwi, Mohammed Rashid na Adam Salamba.
Simba itakuwa na mzigo wa kusaka alama nyingine tatu baada ya kushindwa kuzipata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Nanda FC huko Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.