Lulu Diva Afunguka Kumtambulisha Mchumba Wake - MULO ENTERTAINER

Latest

23 Mar 2019

Lulu Diva Afunguka Kumtambulisha Mchumba Wake

Lulu Diva Afunguka Kumtambulisha Mchumba Wake
DAR ES SALAAM: Sexy lady kwenye Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka juu ya kumtambulisha mwanaume ambaye yupo naye kwenye uhusiano na kusema hawezi kufanya katika mitandao.


Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Lulu Diva alisema hapendi kuonekana kicheche ndiyo maana anaepuka kumtambulisha kila mwanaume anayekuwa naye kwenye uhusiano ila mwanaume pekee atakayemtambulisha ni mume wake.


“Siyo kwamba sipendi watu wamjue mtu ambaye nipo naye, lakini siwezi kumtambulisha huyu kesho nimtambulishe huyu. Kama mnavyojua, mapenzi siku hizi hayadumu kabisa na watu wataniona mwingi ndiyo maana mwanaume pekee ambaye nitakuja kumtambulisha ni mume wangu,” alisema Lulu Diva.