Polisi awapa kichapo Trafiki - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Mar 2019

Polisi awapa kichapo Trafiki


Maafisa wawili wa Trafiki katika barabara ya Port-Bumala nchini Kenya wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa afisa wa polisi mmoja wa kikosi cha kupambana na ghasia 'General Service Unit (GSU)'.

Katika ripoti iliyochapishwa na Citizen tukio limetokea Jumanne, Machi 5, 2019 mchana baada ya afisa huyo wa usalama (GSU), ambaye alikuwa anapita katika kizuizi hicho kuwasema maafisa hao wa trafiki baada ya kushuhudia askari wenzake hao wakipokea rushwa  kutoka kwa mwendesha bodaboda.

Kwa mujibu mmoja wa walioshuhudia tukio hilo, afisa huyo wa GSU ambaye ni mkazi wa eneo la Funyula, aliwatandika maafisa hao wote wawili, wakati walipomvamia kwa pamoja na kuwalazimu kukimbilia katika eneo la Sio Port walipozidiwa na kichapo.

Inakisiwa kuwa, Onyango alipatwa na majeraha ya kichwani ambapo alitibiwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Sio Port na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Hata hivyo, kamanda wa polisi wa eneo la Busia, John Nyoike, amedhibitisha kisa hicho na kufichua kuwa uchunguzi dhidi ya maafisa hao ambao wanavalia sare za raia umeanzishwa.