JPM Amfuatilia Aliyelawiti Mtoto, Amkuta Gerezani, Ahukumiwa Maisha - MULO ENTERTAINER

Latest

27 Apr 2019

JPM Amfuatilia Aliyelawiti Mtoto, Amkuta Gerezani, Ahukumiwa Maisha

Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ameagiza uongozi wa Mkoa wa Mbeya kushughulikia matibabu ya mtoto wa miaka sita aliyelawitiwa na mze wa miaka 53 na kumsababishia madhara makubwa, huku akiagiza kupelekea jina la hakimu aliyehukumu kesi hiyo na kumfunga maisha mtuhumiwa wa kesi hiyo.

Magufuli ameagiza hayo leo, Jumamosi, Aprili 27, 2019 wakati akiwahutubia wananchi wa chunya kwenye uzinduzi wa Barabara ya chunya Mbeya na uekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa barabara ya chunya Makosngorosi uliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Chunya.

“Hili la ubakaji linataka kuwa ugonjwa katika maeneo haya, jana wakati wa mkutano wangu Mbeya, mama Swaumu Satimani Mwalembe alieleza shida yake kwamba mtoto wake (aliyekuwa na miaka sita kipindi hicho) alilawitiwa na Idd Said Sekeni, kesi ilipoanza kukawa na ujanja ujanja, wakati mwingine akienda kwenye vyombo anawekwa ndani.

“Alikwenda kwa RC Abbas Kandoro (marehemu) ambaye aliipeleka kesi hii ikashughulikiwa vizuri. Ikamkuta hakimu anaiwa Mteite, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, akatumia sheria zote, licha ya yule mhalifu kuficha lakini hakimu aliiendesha ile kesi na akahumkumu kifungo cha maisha jela.,

“Kwa sababu alihukumiwa akiwa hayupo, nimetuma watu wangu kufuatilia, wamemkuta kwenye Gereza la Luanda, na picha yake nimeletewa anatumikia kifungo cha maisha. Nimpongze sana hakimu Mteite, ninaagiza jina la huyu hakimu lipelekwe kwenye mapendekezo kwa Jaji Mkuu, kwenye majina yatayokuja kwa ajili ya kuteuliwa ujaji na la kwake liwemo.

“Naipongeza sana mahakama kwa kusimammia sheria na vyombo vyote vya dola kwa kufanya kazi vizuri. Asingekua amepatikana huyu mtuhumiwa maagizo yangu ya leo yalikuwa tofauti sana.

“Kwa yule mtoto aliyelawitiwa, nauomba uongozi wa mkioa umpeleke hospitali kwa gharama za Serikali, akachunguzwe na kutibiwa, sasa hivi ana miaka tisa lakini hali yake siyo znuri, anatoka haja mfululizo, naomba mshughulikie matibabu yake na kama hajaanza shule apelekw ssasa hivi aanze kusoma,” amesema Magufuli.