Kwanza naomba ni declare interest kuwa mimi ni shabiki wa maendeleo katika nyanja zote. Lakini kwa leo nitazungumzia muziki wetu hapa nchini (Bongoflava). Lakini point yangu nitaielekeza haswa kwa mafahali wawili, yaani Diamond na Slikiba.
na nitachukua reference ya show ya Kiboko Yao iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo, iliyofanyika jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya leaders.
Ni ukweli usiofichika kwamba wasanii wote waliotumbuiza walijitaidi kwa kiwango kikubwa sana, hongera sana kwani kuna changes kubwa sana. Lakini kuna jambo halikuwa sawa katika show ile, alo ni kurushwa makopo stejini wakati Diamond akitumbuiza na hapo ndio hoja yangu inapojengeka.
Bila kuwachosha sana, Diamond ametuwakilisha Watanzania kwenye shoo nyingi za kimataifa, ni nyingi siwezi kuzitaja zote, mbona Wanigeria, Marekani, Canada, Germany, Rwanda, Burundi etc hawakumrushia makopo? Kwanini itokee nyumbani Tanzania? Ni wivu au chuki kiasi gani juu ya msanii huyu mwenye kuheshimika Afrika kwa sasa? Amewakosea Watanzania?
Natambua Watanzania wengi hatupendi kuona mtu anaendelea, tumezoea majungu, fitina, chuki, umbea, na wivu. Jamani tubadilikeni. Maskini ya mungu Diamond huna ugomvi nae unamchukia kwanini? Au alikikiba hata hujawai kumuona unamchukia kakukosea nini?
Nimetafakari nikagundua ndio mana tuko nyuma in everything. Nenda Kenya and see how Jaguar anathaminiwa nchini mwao, Go Uganda and see how Jose Chamilione is respected. Hivi vitu vya team ujinga in negative way ni ushamba uliopita kiwango, inatakiwa team in constructive way.
Tunaomba Alikiba na Daimond washirikiane kuendeleza muziki wetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Samahanini kwa kuwachosha. Asanteni kwa kunisoma.
29 Jan 2015
New