Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar
nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae
amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu
walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.
Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi
chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia
gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya
kupangisha.
Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana
elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka
kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani
kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi
mpya ambae anaelimu ya chuo sio mshamba kama huyu wa zamani.
Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari
kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?
11 Jan 2015
New
Mapenzi>>Amenisomesha, Gari kaninunulia lakini sina Mapenzi Naye kabisaaaaaa..Nifanyeje?
mulo