Udaku>>Jack Wolper Nusura Azue tafrani katika Uhusihano wa Nay wa Mitego Kwa Siwema - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Jan 2015

Udaku>>Jack Wolper Nusura Azue tafrani katika Uhusihano wa Nay wa Mitego Kwa Siwema


KIMENUKA! Mwigizaji Jacqueline Wolper ameibua tafrani la aina yake kwa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kumtumia meseji iliyomtia shaka mpenzi wa staa huyo, Siwema.

Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara- Korogwe jijini Dar  ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa ikiuliza muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza kumcharukia bebi wake huyo.

Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:
“Wolper ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita maelezo, hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema dizaini kama alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na kila kitu kipo sawa.”