BAADA ya msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga kutangaza nia ya
kutaka kumposa mwigizaji Jacqueline Wolper, staa huyo ameibuka na
kumjibu kuwa na yeye yupo tayari kama ataweza kutimiza masharti.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema katika mila za Kiafrika,
posa haikataliwi, inatolewa na kisha inajadiliwa kwa hiyo kama Manaiki
kajipanga, apeleke posa ikajadiliwe na wazee wake.
“Nimesikia habari za Manaiki kutaka kuniposa nikacheka sana kwa sababu
yeye kama yupo tayari apeleke posa itapokelewa kwani siku zote vigezo na
masharti huzingatiwa, afuate utaratibu tu,” alisema Wolper.
12 Jan 2015
New
Mapenzi>>Jackline Wolper Akubali Kuposwa, ila Masharti na Vigezo Kuzingatiwa
mulo