Polisi nchini Kenya wanasema afisa mmoja wa kanisa amepigwa risasi na kuuawa alipokuwa akielekea katika maombi.
Madhumuni ya mauaji hayo hayajatambulika, lakini Muungano wa Makanisa mjini Mombasa tayari umesema ni mauji ya kidini.
Mauaji ya afisa wa kanisa jijini Mombasa yanatishia kuhangaisha wakaazi
walioanza mwaka kwa amani baada ya machafuko mengi ya mwaka 2014.
Polisi wanasema afisa wa kanisa moja jijini Mombasa alipigwa risasi na
kufariki alipokuwa akiingia ndani ya shule moja ambayo wameikodisha
kufanya maombi yao.
Mkuu wa Upelelezi wa Uhalifu Mombasa Ondiek amesema mtu mmoja aliyekuwa
na bunduki alimfuata jamaa huyo hadi akaingia ndani ya uwanja wa shule
kabla ya kumpiga risasi. Alikufa papo hapo.
Aidha Ondiek amesema Polisi waliokuwa wameshika doria shuleni walisikia
sauti za risasi na hivyobasi kumkabili muuaji huyo, lakini akahepa ndani
ya vitongoji vilivyo karibu na shule.
11 Jan 2015
New
Siasa>>Mauaji Mengine Kenya Mombasa, Sasa yamehamia Kanisani..
mulo