Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ufafanuzi wa sakata la uchotaji fedha
kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu na kutangaza
kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya viongozi na watendaji, nchi wahisani
wamesema bado suala hilo linawachanganya na wanasubiri tamko la
Serikali.
Nchi hizo, ambazo zilizuia takriban Sh1 trilioni za ufadhili na
kuchangia nakisi ya bajeti ya Serikali, juzi zilikiri kuanza kuruhusu
sehemu ya fedha hizo baada ya baadhi ya maazimio ya Bunge la Jamhuri ya
Muungano kuanza kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na kumvua uwaziri Anna
Tibaijuka, kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Eliakim Maswi na kumuweka kiporo waziri wake, Sospeter Muhongo na
kusababisha Jaji Fredrick Werema kujivua wadhifa wake wa Mwanasheria
Mkuu.
Tayari Rais Jakaya Kikwete ameshaeleza kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili juzi, Balozi wa Jumuiya ya Ulaya
nchini, Timothy Clarke alisema kwamba Serikali imeonyesha jitihada za
mwanzo, lakini wanasubiri kuona hatua kali zaidi zikichukuliwa pamoja na
kuja na kauli moja kuhusu fedha hizo.
Alisema alichobaini ni kwamba wananchi wengi wanataka kujua hatima ya
sakata hilo ndiyo maana walitumia vyombo vya habari kufanya mijadala
mbalimbali kuzungumzia wizi wa fedha za escrow ambazo haijawekwa wazi
kuwa ni za umma ama ni za Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL
11 Jan 2015
New
Siasa>>SAKATA LA IPTL: Mabalozi waitaka Serikali kuchukua hatua kali
mulo