Uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita umeonyesha rangi halisi ya CCM na viongozi wake.
Mtaa wa Kigogo Fresh B Pugu-Ukonga anaishi Waziri mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda.Siku ya uchaguzi tarehe 14 December uchaguzi ulivurugika haukufanyika na mkurugenzi akatangaza ungefanyika wiki moja baadaye.
Mgombea wa Chadema aliaminiwa na wananchi wa mtaa huu kwa sababu anayajua matatizo ya watu wa Pugu.Wananchi walitaka kumpa ushindi wa zaidi ya asilimia 90% uchaguzi ungefanyika.Mgombea wa CCM alishindwa hata kufanya mkutano wa wazi kwa sababu kila alikokuwa anapita anazomewa na hata watoto wadogo.
Hata hivyo siku moja kabla ya uchaguzi wa Marudio mkurugenzi wa Ilala akiwa amejifungia ofisini alimtangaza mgombea wa CCM kwamba ndiye mwenyekiti mpya wa mtaa wa Kigogo Fresh B bila ya uchaguzi.
Tangazo hili lilileta hasira kubwa kwa wakazi wa mtaa huu na wakaamua siku ya kuwaapisha kutumia nguvu ya Umma kumzuia mkurugenzi kufanya uhuni huu.Na kweli mkurugenzi akashindwa na kuahirisha zoezi.
Sasa kuna taarifa kwamba wakubwa wameamua ni lazima wamuapishe mtu wao waliyemuweka madarakani kwa njia ya mapinduzi.Kwamba ataapishwa leo Alhamisi tarehe 22/1/2015 saa 3 asubuhi katika ukumbi wa Anatougle kwa sababu Waziri mkuu kamwe hawezi kuongozwa na Chadema mtaani kwake.
Wananchi wa Kigogo Fresh B wamesema kamwe hawatakubali udikteta huu kwenye mtaa wao.
Tusubiri tuone....
22 Jan 2015
New