Aibu:Ripoti ya PCCB yafichwa Kulinda Familia Kuu Sakata la ESCROW - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Feb 2015

Aibu:Ripoti ya PCCB yafichwa Kulinda Familia Kuu Sakata la ESCROW

Ni aibu kwamba mjadala wa escrow unaelekea kufa bila watanzania kujua kwa hakika mgao wa Singasinga alimpa nani wakati ndioa asilimia 70 ya pesa za ESCROW.
Waliofahamika ni waliopata mgawo kutoka kwa Rugemalila aliyepata asilimia 30 tu ya pesa za..
Escrow. Na majina yao yamepatikana kupitia akaunt ya Rugemalila pale Mkomboz Bank.

Tukumbuke kuwa pale Stanbic ndio zilitolewa bilion 73 cash kitu ambacho kinyume cha sheria za fedha nchini, lakini mpaka sasa hawajulikan waliogawana na Usalama wa Taifa wametia ngumu kuhakikisha hakuna mjadala kuhusu hilo.

Bunge lilokwisha Kafulila alipeleka hoja binafsi kutaka ripoti ya PCCB ijadiliwe bungeni kama ilivyoahidiwa na Pinda mwenyewe Bunge la may 2014 kuwa ripoti zote za uchunguzi za CAG na PCCB zingejadiliwa na bunge liamue.

Lakini cha kushangaza Ofisi ya Spika imetupilia mbali hoja ya kutaka ripoti ya PCCB ijadiliwe kwa madai kwamba kanuni haziruhusu kujadili hoja iliyokwisha amuliwa na Bunge mpaka baada ya miezi 12.

Ukweli ni kwamba hoja iliyofanyiwa mamuzi na Bunge ni ripoti ya CAG kuhusu muamala wa ESCROW na sio ripoti ya PCCB kuhusu muamala wa ESCROW. hizi ni hoja mbili tofauti..

Ripoti ya PCCB imekaanga kuanzia ikulu mpaka chini kwa majina. Imekaanga familia ya Rais. Na ikiwekwa wazi mtikisiko wake haujapata kutokea. Ndio sababu ya jitihada kubwa za baadhi ya watu wa usalama kudhibiti mjadala wa ESCROW kuhusu zilikokwenda asilimia 70 ya pesa hizo.

Kumbuka tu Hosea kwasasa ni Makam Mwenyekiti wa Anti corruption body duniani na pia ndiye Rais wa Anti corruption body Africa na SADC. Hana cha kupoteza Tanzania. Ndio maana ripoti alotoa imekaliwa Ikulu.