Baada ya Kupigana Kibuti Isabelah Atoa Siri Kuhusu Kuharibika Kwa Mimba Nne za Kalama, Asema Damu zao zilikuwa Haziendani - MULO ENTERTAINER

Latest

3 Feb 2015

Baada ya Kupigana Kibuti Isabelah Atoa Siri Kuhusu Kuharibika Kwa Mimba Nne za Kalama, Asema Damu zao zilikuwa Haziendani

BAADA ya kuachana rasmi mwanzoni mwa mwaka huu, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Luteni Karama,msanii huyo wa kike ameamua kumwaga mchele kwa kudai kuwa aliwahi kushika mimba zaidi...

ya nne za Karama na zote zikaharibika.

Akifunguka mbele ya paparazi wetu, Bela alisema alikuwa akishika mimba hizo lakini zote zilikuwa zikiharibika baada ya kufikisha miezi minne tu.

“Nilikuwa napenda kumzalia Karama lakini kila alipokuwa akinipa mimba zote zilikuwa zikiharibika, ameshanipa mimba nne na zote zikawa hivyohivyo. Sijui lakini labda damu zetu zilikuwa haziendani kwenye mimba,” alisema Bela.