Baada ya Vurugu na Vituko Vingi Mjini eti Mwanamuziki BABY MADAHA Nae Anatamani Kuitwa Mama Sasa - MULO ENTERTAINER

Latest

6 Feb 2015

Baada ya Vurugu na Vituko Vingi Mjini eti Mwanamuziki BABY MADAHA Nae Anatamani Kuitwa Mama Sasa

 MWIGIZAJI na msanii wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha, amesema anatamani kuitwa mama kama ilivyo kwa wanawake wengine wenye watoto.



Akizungumzia swala hili, Baby Madaha, alisema amepanga kufanikisha ndoto zake za kuwa mama mwaka huu. “Kiukweli natamani sana kupata mtoto, nafarijika nikisikia na kuona wenzangu wanaitwa mama, ni jambo la busara na kumuomba Mungu ili litimie,” alisema Baby Madaha.

Madaha alisema wasanii wengi wamefululiza kuzaa jambo ambalo linapendeza katika jamii, lakini uamuzi wake si wakufuata mkumbo kama ambavyo wengi watafikiria.