Rose Ndauka asema sitozaa tena nje ya ndoa... - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Feb 2015

Rose Ndauka asema sitozaa tena nje ya ndoa...

Stori: 
DIVA wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amefunguka kuwa alikosea kuzaa nje ya ndoa, na sasa hana mpango huo tena.
Rose alisema suala la ujauzito wakati mwingine linaweza kumjia mtu bila kupenda lakini kwa sasa atajitahidi kuona anazaa akiwa ndani ya ndoa.
Diva wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
“Lolote linaweza kutokea lakini kiukweli kwa sasa nitakuwa makini kidogo na ninamuomba Mungu anisaidie mtoto wa pili nimzalie ndani ya ndoa,” alisema Rose ambaye alizaa na Mbongo Fleva, Malick Bandawe kisha kumwagana.
Mwigizaji huyo kwa sasa ameandaa jarida lake ambalo litakuwa linatoka mtaani kila Jumatatu.