UNATAKA SIX PACKS(TUMBO LA MAZOEZI) NA KUWA NA MVUTO WA MAPENZI...FANYA HIVI. - MULO ENTERTAINER

Latest

27 Feb 2015

UNATAKA SIX PACKS(TUMBO LA MAZOEZI) NA KUWA NA MVUTO WA MAPENZI...FANYA HIVI.

Tumbo la zoezi lilogawanyika na kujitengeneza pakti sita linahitaji mazoezi ya kutosha na siyo kitu cha kuja usiku mmoja, bali ni kwa mazoezi endelevu na ukiweza kumudu kufanya haya mazoezi utaona matokeo yake". 
 Kwa tumbo kukatika katika na kutoa mistari wanawake wanayoiona ni ya kimahaba, waulizewanaume wamekukusanyia mazoezi ambayo yatakuletea maajabu na kulibadilisha tumbo lako kuwa tofauti na kukufanya utembee kifua wazi...


RATIBA YA MAZOEZI>>


  1. Fanya mazoezi haya mara mbili kwa wiki.
  2. Chukua mapumziko ya dakika 15 mpaka 30 kwa kila seti ya mzunguko wa mazoezi.
  3. Chukua pumziko la dakika 60 kwa kila zoezi.
             1; Suspended Reverse Crush
  Kwa hili zoezi, funga kamba mwisho mwa miguu yako yote miwili, huku ukiwa kwenye mkao wa pushapu, kunja miguu na rudisha kwa urefu kama picha inavyoonesha.
>Fanya seti tano.
>Seti ya kwanza mara 15,
>Seti ya pili mara 12,
>Seti ya tatu mara 10,
>Seti ya nne mara 10,
>Seti ya tano mara 10.

             2; Decline Russian Twist

Kaa wima kwenye kiti kilicho binuka kwenye engo ya nyuzi 45, jizungushe upande wa kuria na wa kushoto huku umebeba chuma chenye uzito mdogo kama picha inavyoonyesha.
>Fanya seti 5.
>Rudia mara 12 kwa kila seti.

            3; Hanging Leg Raises

 Bembea kwenye chuma na nyanyua miguu kufikia urefu sambamba na wa kiuno chako, huku mwili wote ukibaki wima kama picha inavyoonyesha.
>Fanya seti 5,
>Rudia mara 12 kwa seti zote.

Hakikisha unazingatia ratiba ya mazoezi.

  1. Fanya mazoezi haya mara mbili kwa wiki.
  2. Chukua mapumziko ya dakika 15 mpaka 30 kwa kila seti ya mzunguko wa mazoezi.
  3. Chukua pumziko la dakika 60 kwa kila zoezi.