Escrow: Stanbic Bank Kuchafua Hali ya Hewa..Kutaja Majina ya Waliobeba Mahela Kwa Lumbesa - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Mar 2015

Escrow: Stanbic Bank Kuchafua Hali ya Hewa..Kutaja Majina ya Waliobeba Mahela Kwa Lumbesa

Nimepenyezewa taarifa na mnene mmoja wa Stanbic kuwa Viongozi waandamizi wa Stanbic Bank huko majuu wanakaribia kuchafua tena hewa ya nchi.Waandamizi hao wameagiza kuanikwa kwa majina ya waliochota malumbesa ya fedha za Escrow. Wamewaagiza wakuu wa hapa Tanzania kuhakikisha ifikapo Aprili mosi mwaka huu,majina hayo yawe public pamoja na mihamala yao ili kusafisha taswira ya Stanbic.

Ukisikia kusafisha hapa na kuchafua pale ndio huku.Siombi hilo litokee.Hawa wa Mkombozi Bank aka wa Rugemalira wametuhenyesha hivi.Wa Stanbic itakuwaje? Stanbic Bank,please and please, re-think and re-decide. Tumechoka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam