Jihad John |
BBC News imeripoti leo kuwa Waziri Chikawe amesema kuwa Johad John alitaka kufanya vitendo vya ugaidi nchini Tanzania. Akiongea na correspondent wa BBC Afrika Mashariki Ed Thomas, Waziri Chikawe amesema kuwa hakukuwa na tip-off yoyote kutoka kokote kumzua Jihad John kuingia nchini, lakini alitaka kutudhuru. Kwa maneno ya Kiingereza Waziri amesema:
Jihad John |
Report ya Polis wa Airport Baada ya kumkamata Jihad John |
My Take:
Maelezo ya Waziri yanaleta maswali mengi. Mojawapo ni kama Jihad John angekuwa hajalewa, kama alikuwa hajawatukana maasifa wa uhamiaji pale uwanjani kana inavyodaiwa, bado angeruhusiwa kuingia nchini pamoja na kuwa Waziri anaamini Emwazi alitaka kutudhuru aka "wanted to harm us"?
Pili, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Ernest Mangu, ashaliambia gazeti la The Citizen kuwa jina la Mohammed Emwazi halikuwepo kwenye database ya watuhumiwa wa kigeni waliokamatwa na kuondolewa nchini mwaka 2009 (IGP: Jina la Mohammed Emwazi halikuwepo kwenye database ya polisi). Kanusho hilo liliripotowa pia na BBC News. Ina maana IGP alidanganya au alikuwa hajuia alichokuwa anakisema? Kwa nini serikali inajichanganya sana kwenye hili suala la Jihad John? Au ni vyombo vya habari vinawanukuhu vibaya?