BREAKING NEWS: WACHIMBAJI WADOGO WADOGO 19 WA DHAHABU WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNUKWA NA KIFUSI WILAYANI KAHAMA - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Apr 2015

BREAKING NEWS: WACHIMBAJI WADOGO WADOGO 19 WA DHAHABU WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNUKWA NA KIFUSI WILAYANI KAHAMA

Wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo ya kijiji cha karore kata ya Runguya tarafa ya msalala wilaya ya kahama mkoani Shinyanga.

Kwamujibu wa Kamanda wa polisi mkoani humo Justus Kamugisha Amesema usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivavamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.