Jini Kabula Ataja Mchawi wa Soko la Filamu - MULO ENTERTAINER

Latest

30 Apr 2015

Jini Kabula Ataja Mchawi wa Soko la Filamu

Staa mrembo wa Bongo Movies,  Mariam Jolwa ‘Jini Kabula’ amesema kuwa anguko la soko la filamu za Bongo asitafutwe mchawi, kwani wasanii wengi wanaigiza chini ya kiwango na ndiyo maana kazi zao hazifanyi vizuri, licha ya kutumia gharama kubwa kuziandaa.                                       

Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Dar es Salaam jana, Jini Kabula alisema kuwa ni filamu chache zinazofanya vizuri sokoni, ikiwemo ya Chozi la Wanjaa iliyochezwa na Aunt Ezekiel, Kulwa Kikumbi ‘Dude’ na wasanii wengine ambazo zinaonekana kuwafurahisha watu, isipokuwa nyingi zinatengenezwa kwa kulipuliwa.
Hakuna haja ya kumtafuta mchawi wa anguko la filamu nchini, kwani wengi wanatengeneza kwa kulipua, endapo waandaaji wasipobadilika, fani hii itakuwa haina maana tena kwa waigizaji,” alisema.