BAADA ya Simba kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyopigwa uwanja wa Sokoine mwishoni mwa juma lililopita, kipa kijana wa Msimbazi, Manyika Peter Jr alilaumiwa na mashambiki kwa kudaka chini ya kiwango.
Mashabiki hawakuridhishwa na udakaji wake na kudai ameshuka kiwango tangu awe katika mahusiano ya kimapenzi na Mrembo mmoja anayeitwa Naima.
Baada ya lawama kijana Manyika Jr alikuja juu na kutoa majibu yanayoonekana pichani chini kwa mashabiki wa Simba wamamshutumu kushuka kiwango kwasababu ya mapenzi.