Mdau amewasilisha baadhi ya hoja akizungumzia dalili ambazo zinaweza kuwa taarifa kama mtoto anatumika kingono. Hoja zake ni;
Mtoto kupata shida wakati wa kukaa au kutembea (miaka 2 - 10) na kuwaogopa baadhi ya watu kupita kiasi au sehemu fulani au vitu (miaka 0-5)
Mtoto kupenda kujishika sehemu za siri kiasi cha kujisahau mpaka kulala akiwa anajishika na kukaa chooni muda mrefu au kuhitaji kujisaidia mara kwa mara (miaka 0-5)
Anaweweseka usiku (miaka 0-5), anakataa/kusumbua kula au kutapika bila ugonjwa mahususi (miaka 0-5) na huona aibu na kujitenga (umri wote)
Hushindwa kuzuia haja kubwa (miaka 4-7), kuwa mkimya isivyo kawaida (umri wa balehe), kuwa na kiburi, maamuzi ya kukinzana na maagizo ( umri wa balehe) na kuwa na Msongo wa mawazo (8-17)
Je, wewe wafahamu nyingine? Tufahamishe