Mgomo Wa Madereva: Mbowe Apokelewa Kwa Shangwe Na Madereva Waliogoma Ubungo, Aokoa Jahazi na Mgomo Kwisha - MULO ENTERTAINER

Latest

6 May 2015

Mgomo Wa Madereva: Mbowe Apokelewa Kwa Shangwe Na Madereva Waliogoma Ubungo, Aokoa Jahazi na Mgomo Kwisha

Mgomo umesitushwa. Mbowe kaokoa jahazi. Kikao cha kwanza kilikuwa cha DC Makonda. Fujo zikazuka hadi polisi wakaingilia kwa kufyatua silaha zao. Baadaye akaingia Mbowe na watu wakamsikiliza. Kilichoishinda Serikali kwa siku mbili kimemalizwa na mtu mmoja kwa dakika 7. Mtu ambaye hana hata polisi, achilia mbali jeshi
Mbowe kawaambia sentensi moja tu... "Serikali iliyopo haina uwezo wa kutatua matatizo sio ya nyie tu madereva, bali na makundi mengine ya kijamii ikiwemo wakulima, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi, askari nk... hivyo njia pekee ni nyie kuendelea na kazi na kuvumilia miezi michache iliyobaki kisha itaingia serikali makini itatue matatizo yenu".