ALI KIBA Azoa Tuzo Tano Kwa Mpigo Tuzo za Kilimanjaro Music 2015 - MULO ENTERTAINER

Latest

14 Jun 2015

ALI KIBA Azoa Tuzo Tano Kwa Mpigo Tuzo za Kilimanjaro Music 2015

Tuzo za muziki Kilimanjaro, KTMA 2015, zimefanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo Alikiba ameongoza kwa kuchukua tuzo tano.

Joh Makini akiwa mwenye furaha baada ya kukwaa tuzo
Joh Makini ni mmoja wa washindi usiku wa Jumamosi

Tuzo alizoshinda Alikiba ni pamoja na mtumbuizaji bora wa muziki wa kiume, Wimbo bora wa mwaka, mtunzi bora wa mwaka muziki wa bongo fleva, msanii bora wa mwaka pamoja na mwimbaji bora wa kiume wa Bongo Flava.

“Nawashukuru media zote na wote kwa kweli pongezi nyingi zinaenda kwa my strongest #Teamkiba yourthe best #kingkiba_for_life,” ameandika Kiba kwenye Instagram. Msanii huyo kwa sasa yupo Dallas nchini Marekani.

Diamond, Vanessa Mdee, Mzee Yusufu,Isha Mashauzi pamoja na Joh Makini wote wameibuka na tuzo mbili kila mmoja.

“#GODENGINEERING #TEAMWEUSI WE DID IT AGAIN !!! WE WON TWO!! KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS!! THANK Y’ALL FOR VOTE,” ameandika Joh Makini.

Hii ni orodha nzima ya washindi wa KTMA 2015:

Mtumbuizaji bora wa muziki wa kiume wa mwaka – Alikiba

Mwimbaji bora wa kike Bongo Flava ameshinda – Vanessa Mdee

Msanii bora wa kiume Taarab – Mzee Yusuph

Mwimbaji bora wa kike Taarab – Isha Mashauz

Mwimbaji bora wa kiume bendi – Jose Mara

Wimbo bora wa mwaka wa muziki wa Taarab – Mapenzi Hayana Dhamana – Isha Mashauzi

Wimbo bora wa mwaka – Mwana (Alikiba))

Wimbo bora wa Kiswahili bendi – Walewale (FM Academia)

Wimbo bora wa muziki wa R&B – Sisikii (Jux)

Wimbo bora wa Hip Hop – Kipi Sijasikia (Professor Jay)

Wimbo bora wa Reggae & Dance Hall – Let Them Know (Maua Sama)

Rapper bora wa mwaka, bendi – Ferguson

Msanii bora wa Hip Hop – Joh Makini

Wimbo bora wa Afrika Mashariki – Sura Yako (Sauti Sol)

Mtunzi bora wa mwaka, Taarab – Mzee Yusuph

Mtunzi bora wa mwaka, Bongo Flava – Alikiba

Mtunzi bora wa mwaka, bendi – Jose Mara

Msanii bora chipukizi – Baraka Da Prince

Mtunzi bora wa mwaka Hip Hop – Joh Makini

Bendi bora ya mwaka – FM Academia

Mtayarishaji bora wa nyimbo, Bongo Flava – Nahreel

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka, Taarab – Enrico

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka, bendi – Amoroso

Wwimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania – Mrisho Mpoto

Kikundi bora cha mwaka muziki wa Taarab – Jahazi Modern Taarab

Kikundi bora cha mwaka muziki wa Bongo Flava – Yamoto Band