Aliyetaka Kumuua Mwanamuziki Lil Wayne Kwa Risasi Akamatwa na Polisi - MULO ENTERTAINER

Latest

2 Jun 2015

Aliyetaka Kumuua Mwanamuziki Lil Wayne Kwa Risasi Akamatwa na Polisi

Polisi kutoka Mji wa Atlanta waperipoti kumkamata mtu aliyejaribu kumuua Mkali wa Hipohop Lil Wayne kwa kupiga risasi basi lake la safari.

Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi wamemtaja mtu huyo anayejulikana kwa jina la Jimmy Carlton Winfrey na ni mtu wa karubu wa Young Thug.

Kwa Mujibu wa maelezo aliyoyatoa kwenye kituo cha polisi baada ya kufanyiwa mahojiano, Jimmy Carlton Winfrey alisema aliamua kupiga basi hilo ili pate heshima ndani ya kundi lake la Bloods Gang.

Bado hukumu yoyote haijatolewa na polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi ambapo kesi hiyo itapandishwa mahakani kwa ajili ya kutoa hukumu.

Wiki kadhaa zilizopita iliripotiwa kupigwa risasi basi la Lil Wayne lillokuwa likipita kwenye mji wa Atlanta huko Marekani, mji ambao anaishi hasimu wake mkubwa kwa sasa Young Thug.

Kumekuwa na taarifa za kupeana vitisho vya kutoana uhai kwa wasanii Lil Wayne na Young Thug ambao wanaonekana kuingiliana kwenye biashara za muziki wanao ufanya.