Breaking News. - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Jun 2015

Breaking News.


Habari za hivi punde zilizokifikia chumba cha habari kutoka Mkoani Geita ni kwamba mtangaza nia kugombea nafasi ya

udiwani kata Rwamgasa wilaya ya Geita na Ubunge jimbo la Busanda  mkoani Geita kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Paulo Ntilima ( 30)  amecharangwa  mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wasiojulikana usiku huu.

Malunde1 blog imeambiwa kuwa mtia nia huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Rwamgsa kata ya Rwamgasa wilaya ya Geita amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani na hali yake inadaiwa kuwa ni mbaya.

Mwandishi wa Malunde1 blog mkoani Geita Valence Robert ambaye amefika eneo la tukio anasema mtia nia huyo amelazwa wodi namba 8 hospitali  ya wilaya ya Geita kwa ajili ya matibabu.
HABARI KAMILI TUTAKUPATIA HIVI PUNDE!