Mshiriki wa BBA Kutoka Namibia Amwagia Sifa Wema Sepetu - MULO ENTERTAINER

Latest

2 Jun 2015

Mshiriki wa BBA Kutoka Namibia Amwagia Sifa Wema Sepetu

Mshiriki wa Big Brother Afrika ‘BBA’ Hot Shot 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Munana, amemwagia sifa aliyekuwa Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu kuwa ni mwenye mvuto wa kipekee.

Lakini licha ya kutoa sifa hizo, mshiriki mwenzao ambaye ndiye mwenyeji wao, Idris Sultan, hakutokea katika sherehe hiyo jambo lililozua minong’ono kwa watu baada ya tetesi kwamba ana ugomvi na Wema Sepetu.

Wema alimwagiwa sifa hizo alipokuwa katika sherehe za Instagram Party katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

“Wasanii ninaowakubali kutoka Tanzania ni Wema Sepetu, ni mrembo sana nampenda, wasanii wengine ambao nawakubali ni Shilole, Ommy Dimpoz pamoja na wimbo wake wa Wanjera,” alisema.
Washiriki wengine wa BBA waliohudhuria sherehe hizo ni Nhalanhla na Samantha wote kutoka nchini Afrika Kusini.

Wasanii wa Tanzania waliohudhuria sherehe hiyo ni Ben Paul, Izzo Bizness, Shelta, King Majuto, Stan Bakora, JJ Band, huku mshereheshaji akiwa Adam Mchomvu, B Dozen na DJ Ommy.
Hata hivyo, Wema alishukuru kupendwa na Luis. “Jamanii sina hata la kusema jinsi ulivyonisifia, nashukuru sana sana,” alijinadi Wema akishukuru.