Wema Sepetu Akiri Kutoa Mimba, Sheria za Nchi Zinasemaje? - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Jun 2015

Wema Sepetu Akiri Kutoa Mimba, Sheria za Nchi Zinasemaje?

Wema Sepetu Akiri Kutoa Mimba, Sheria za Nchi Zinasemaje?
Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Take One hapo jana amekiri kuwa alitoa mimba maana hakuwa tayari kwa wakati ule.Ilikuwa mwaka 2008 na mimba ilikuwa ya marehemu Steven Kanumba

Kanumba alikuwa akimwambia kuwa nitakudai watoto wangu, kauli hii inamaanisha kuwa alitoa mimba zaidi ya moja.

Akizungumzia kuhusu kupata mtoto amesema anatamani sana kuwa na mtoto lakini ndio hivyo tena kahangaika sana lakini hajafanikiwa.Anadai labda wakati anatoa kuna vitu viliguswa ndio maana hafanikiwi kupata mtoto.

Anasema anajuta/hajuti kukosa mtoto.

Pia amekiri alihongwa BMW,kuhusu MURANO anasema lilikuwa na matatizo ya shockup na halikuwa katika hali nzuri.
Sheria za Tanzania haziruhusu suala la Utoaji wa mimba katika Criminal Procdure Act ,1985 .
Katika sheria hio hio suala hili limejumuishwa katika makosa ya "Murder" ambayo makosa yake yanaweza kwenda kifungo cha maisha au kifo

Katika jedwali la Adhabu inaonesha adhabu zifuatazo kwa watu wanaotoa au kushiriki kutoa Mimba
  • 150.Attempt to procure abortion. -Imprisonment for fourteen years.
  • 151.Woman attempting to procure her own abortion. -Imprisonment for seven years.
  • 152.Supplying drugs or instruments to procure abortion. -Imprisonment for three years
Katika jamii yetu kuna watu ambao aidha kwa mazuri au mabaya yao wamekuwa wakiangaliwa na watu wengi.Vyombo vya habari pia vimekuwa vikiuza kwa kuwataja kutokana na scandals zao.

Hapa namwongelea Wema Sepetu ambaye yeye pia anaandikwa sana hasa na Magazeti ya "Udaku"

Magazeti haya yanasomwa sana na jamii kubwa ya watanzania hasa kutokana na hali zetu za elimu na "mazingira"

Huyu Binti amefikia hatua ya Kusema "Proudly" kuwa alitoa mimba kwa sababu hakuwa tayari,hili amelisema wakati akihojiwa na mtangazaji Zamaradi mketema wa Clouds TV;

Implication yake ni nini?
  1. Kwa wale wasio na uelewa mpana wataona kwamba ni sawa tu kutoa mimba kwa sababu wema ameongea proudly NA hakuna kilichofanyika
  2. Serikali inadhalilishwa wazi kuwa watu wanapigia kampeni suala la utoaji wa mimba kuwa ni halali tu
  3. Taasisi za Haki za binadamu hazifanyi kazi ipasavyo kiasi cha watu kama hawa kuachwa bila kukemewa.Huyu binti ameua na amekiri kwa mdomo wake kuua.
  4. Vyombo vya haki ya mama na Mtoto vinashindwa kuchukua hatua stahiki hata katika mazingira yaliyo wazi