Aunt Ezekiel: Nimeamua Kuhama CHADEMA Na Kurudi CCM Baada ya Kuvutiwa na Sera za Chama........Sijapewa Pesa wala Gari - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2015

Aunt Ezekiel: Nimeamua Kuhama CHADEMA Na Kurudi CCM Baada ya Kuvutiwa na Sera za Chama........Sijapewa Pesa wala Gari

MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, amedai kutishiwa amani baada ya kufanya maamuzi yake kisiasa ambapo amehamisha ushabiki wake kutoka CHADEMA  na kwenda CCM.

Licha ya mrembo huyo kudai kupokea vitisho mbalimbali, pia alidai amehama chama hicho na kujiunga na CCM kutokana na kukubali sera za chama hicho.

“Sera za chama nilichohamia zimenivutia na wala sikulazimishwa na mtu wala sijapokea fedha wala gari kuhamia huko kama inavyosemekana, bali nafsi na mapenzi pamoja na haki yangu ndiyo yaliyonipeleka huko.

“Nashangaa maamuzi yawe yangu bado watu wanitumie jumbe za vitisho, mimi ni raia kama walivyo wengine, umaarufu wangu usiwe sababu,” alisema Aunt, ambaye awali alikuwa akivaa magwanda  CHADEMA