Akizungumza katika kipindi cha jioni cha E-FM kinachoongozwa na Gadner G. Habash mama mzazi na kaka wa damu wa mwanamuziki fundi na bora wa kizazi cha kati cha watanzania Ramadhani Masanja a.k.a mwalimu wa walimu / Banza stone wamesema kuwa mwanamuziki huyo sasa ni siku ya tatu " hatoi kauli " na " hataki tena kunywa dawa " na " hali yake sasa inazidi kudhoofika " hali inayopelekea wao kukata tamaa na kumwachia mwenyezi mungu.
Hata hivyo mama mzazi wa banza stone aliwashukuru sana wafanyakazi wa kituo cha redio cha e fm na msanii mwenziye muumini mwinjuma kwa kuwa wamekuwa bega kwa bega kujitokeza mara kwa mara kumtembelea na kumsadia mwanamuziki huyo mahiri ambaye binafsi nakiri kuwa huyu jamaa hakika ni " fundi " ktk medani za uimbaji na utunzi na hili halina ubishi.
Kinachonisikitisha sana ni kwamba hata wanamuziki wenzake tu ni kama vile wamemsusa mwenzao ukiachilia mbali huyo muumini mwinjuma na inasemekana kuwa hata wakipigiwa simu hawapokei na wengi wao wanajifanya wapo busy kwenye ma concert yao wakati ukweli ni kwamba wengi wao tunao humu humu mjini.
Hasira yangu kubwa ipo kwa wale mapedeshee wa mjini ambao nakumbuka walikuwa wakimfuata banza stone na kumpigia magoti kuwa awataje katika nyimbo zake kwa mfano " papa antibiotique muzee wa jamii forum mutu ya fedha mingi " ( wakati ukweli hata hizo hela sina ) lakini sasa hata kumsikia tu huyu jamaa aliyekuwa akiwafagilia hawataki na wanamkwepa.
Uchungu wangu mwingine naupeleka kwa marafiki zake ambao wakati ameugua mara ya kwanza na kupata nafuu ndiyo walikuwa wa kwanza kwenda kumchukua na kumpeleka kula nae bata huku wakimpa mipombe, sigarana powder huku wao wakidhani kuwa wanamsaidia kumbe ndiyo wamemfikisha hapa alipo sasa.
Jazba zangu za mwisho nazielekeza kwa wanahabari wa tanzania ambao nina uhakika wengi wao wameweza sana kutengeneza majina yao kupitia mgongo wa banza stone haswa kwa kupata habari zenye mvuto kutoka kwake na nakumbuka kuna tv nyingi sana zilikuwa zinamtumia banza stone kama chambo chao ktk kuvutia watazamaji wao lakini sijaona mwandishi yoyote aliyediriki hata kumpa coverage banza stone juu ya hii hali yake mbaya ya kiafya.
Hitimisho:
Najua wengi sasa tunasubiria tu kwa hamu labda Israeli afanye yake kwa Banza stone ili sasa tuanze kushindana kuvaa suti, madela,miwani huku tukienda na magari yetu ya kifahari msibani, kujifanya ku pledge mahela mengi huku tukitafuta coverage ya kutosha ktk media kwa kujifanya tunamjua sana banza stone na kutoa machozi ya kinafiki nakizandiki.
Najua wengi sasa tunasubiria tu kwa hamu labda Israeli afanye yake kwa Banza stone ili sasa tuanze kushindana kuvaa suti, madela,miwani huku tukienda na magari yetu ya kifahari msibani, kujifanya ku pledge mahela mengi huku tukitafuta coverage ya kutosha ktk media kwa kujifanya tunamjua sana banza stone na kutoa machozi ya kinafiki nakizandiki.
Chonde chonde watanzania wenzangu hali yaBanza stone ni mbaya....narudia nimbaya......na namalizia kusema kuwa nimbaya na naomba uzi wangu huu umguse kila mtu na tujitokezeni kwenda kumjulia tu hali na tuache ushamba kuwa kwenda kumwona mgonjwa ni mpaka uende na kitu ila kwenda kwako tu na maneno yako ya hekima,utu na busara kwa Banza stone kunaweza kumsaidia na akarudi katika hali yake ya kawaida.
Ewe Mwenyezi Mungu mpe nafuu na mjalie afya njema mwanamuziki wetu kipenzi Ramadhani Masanja (Banza stone ) kwani bado tunamujhitaji katika tasnia hii ya muziki wa dansi.
Amina / Amen.