Hatuoni Sababu ya Kutokuchukua Ubingwa - SIMBA - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Jul 2015

Hatuoni Sababu ya Kutokuchukua Ubingwa - SIMBA

Klabu ya Simba imesema hakuna sababu ya wao kushindwa kuchukua kombe la Ligi kuu Soka Tanzania Bara kutokana na kujiimarisha katika nafasi mbalimbali kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa Simba Sc, Haji Manara amesema, wanavijana ambao msimu uliopita hawakuweza kufanya vizuri ambapo kwa msimu ujao watafanya vizuri kwasababu wameshajiandaa vya kutosha na wamekomaa ambao wataungana na wachezaji wazoefu ili kukiimarisha zaidi kikosi hicho.

Manara amesema, usajili wa safari hii umeiweka timu sawa kwa ajili ya kujiweka tayari kuchukua Ubingwa kwani wamejipanga kila eneo kwa ndani na nje ya Uwanja.
Kwa upande wa Usajili, Klabu hiyo imefanikiwa kumsajili Mganda Hamis Kiiza Diego mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia katika mechi za msimu ujao wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.