Huu Ndio Mshahara Mchezaji Ramadhani Singano Anaopewa na AZAM FC Baada ya Simba Kumzengua kwa Mkataba Feki - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Jul 2015

Huu Ndio Mshahara Mchezaji Ramadhani Singano Anaopewa na AZAM FC Baada ya Simba Kumzengua kwa Mkataba Feki

Stori kubwa leo hii  ni aliyekuwa winga wa Simba SC, Ramadhan Singano ‘Messi’ kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Azam fc, ikiwa ni siku mbili tu tangu TFF wavunje mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.
Messi amesaini mkataba mnono kwa dau la milioni 50 na atakuwa analipwa mshahara wa Milioni 2 kwa mwezi.
Kabla ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na Simba, Wekundu wa Msimbazi walitaka winga huyo asaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la milioni 30 na mshahara wa milioni 1.5, lakini alikataa.