Hata Yesu Alipingwa Pia, Usijali Edward Lowassa Kitaeleweka Tu - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Jul 2015

Hata Yesu Alipingwa Pia, Usijali Edward Lowassa Kitaeleweka Tu

Yule Mwalimu Mkuu wa Walimu na Mtakatifu wa Watakatifu kuliko wote waliowahi kuishi Dunia hii na Mwanzilishi wa Dini ya Kikristo, Yesu Kristo pia alipingwa sana kuanzia alivyozaliwa tu watu hasa maelite, Wafalme wenye madaraka makubwa walimpinga, wakamdhihaki na hata kumkamata na kumweka ndani, sasa ni kwa nini walifanya hivyo? ni kwa sababu ya Woga wa mabadiliko, walijua sasa Utawala wao wa dhuluma uko hatarini hivyo haya yanayotokea na anayofanyiwa Bw.Lowasa ni ishara tosha kwangu mimi kama Muumini na mfuasi mkubwa wa Mafundisho ya Mwalimu Yesu Kristo naamini kabisa ya kwamba Bw.Lowasa ndiyo anyefaa klk wote kuiongoza TanZania!

Hapo mwanzo sikumkubali lkn hizi chuki na kampeni chafu anazofanyiwa zimenifanya nijiulize maswali mengi na magumu, ni kwa nini haswa? Kama ni Ufisadi mbona kila anayegombea ana wake, ni kwa nini yeye tu? Hapo ndipo nikajua kuna kitu na siyo Bure!

Dunia nzima haya yanayotokea siyo mageni watu ambao huwa wanakuja kuleta mabadilko huwa wanapingwa kwanza, kuanzia Martini Luther (orijino na siyo mchumia tumbo wa USA) kama vile Mlm.Yesu Kristo pia alipingwa na Kanisa Katoliki na Mapapa wa wakati huo lkn mapendekzo yake Kanisa Katoliki liliyachukuwa na kuyatumia, Mandela alipingwa mpaka na kuwekwa jela leo hii waliompinga, kumkebehi na kumuita Gaidi wameweka sanamu yake kwa kumkumbuka kwenye Miji yao (London)...

Dedicated to Bw. Lowassa!